kwamamaza 7

Jeshi la Burundi wamekanusha kushambulia Rwanda

0

Jeshi la Burundi walito tangazo ikiwa kama ni la kujibu lililo semwa na upande wa Rwanda kuwa watu wenye kuwa na silaha waliingia Rwanda na kuwaua watu wawili na kukimbilia Burundi kama sivyo.

Leo tarehe 13 Mach 2017, wizara ya usalama ya Burundi kupitia ukarasa wa twitter wa msemaji wa jeshi la Burundi Col Baratuza Gaspard alisema ya kuwa hakuna mtu yeyote wa jeshi ao aliyekuwa jeshi aliye onekana akivuka mpaka wa Rwanda na Burundi.

Col Baratuza eti”kupitia tangazo lililotolewa na jeshi la Rwanda na kusema walioua watu Rwanda walikimbilia Burundi, nasi tumependa kujulisha ngazi za nchi hata kimataifa ya kuwa hakuna mtu aliyeonekana akiingia kwenye mpaka wa Rwanda na Burundi”.

Aliendelea na kusema ya kwamba hata siku moja hawatakubali wakosefu ao waharibifu wa usalama wa nchi jirani na kuwapa ukimbizi.

Burundi wamesema ya kuwa wamefanya hayo kwa ajili ya kujibu tangazo lililo tolewa na jeshi la Rwanda kwenye mitandao tarehe 12 Mach 2017, ikisema watu wenye silaha waliingia Rwanda na kuwaua watu wawili na kukimbilia Burundi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.