Swahili
Home » Je,Rwanda na Uganda wangali katika vita baridi? Wadai wasema yafuatayo
HABARI MPYA KIMATAIFA SIASA

Je,Rwanda na Uganda wangali katika vita baridi? Wadai wasema yafuatayo

Kuna taarifa kuwa nchi ya Rwanda na Uganda zingali katika vita baridi kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini Uganda.

Taarifa hizi zinaeleza kuwa chanzo cha kutoelewana huku ni namna ambavyo Uganda inawaunga mkono kisiasa na kiuchumi wapinzani na maadui wakubwa wa serikali ya Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za Chimpreports kupitia upelelezi wake zinafafanua kuwa sababu za kiuchumi baadhi ya zilizozusha swala hili  kwa kueleza  Uganda ilinyima njia ya angani ya kampuni ya Rwandair kwa  kutumia uwanja wa ndege wa Entebbe kufika nchini Uingereza,jambo ambalo harikufurahisha viongozi wa Rwanda.

Viongozi wa Uganda kupitia spika wa CAA,Vianney Lugya walieleza kuwa wanatarajia kuanzisha kampuni yao siku za usoni.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pia,chimpreports imeleza kuwa ushirikiano ni mkia wa mbuzi kuwa kulingana na maneno yake waziri wa ulinzi,Gen.James Kabarebe aliyotangaza kuhusu Uganda aliposema kuwa Uganda ni nchi adui na kuwa Museveni ni mfuasi wa Rwanda kwa maneno tu badala ya vitendo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa hizi zinasema kuwa Kabarebe akiwa kwenye kituo kikuu cha RPF mjini,Kigali eneo la  Gasabo alisema kuwa Uganda inaunga mkono nchi ya Burundi iliyowakaribisha wapinzani wa Serikali ya Rwanda.

Waziri wa ulinzi,Gen.James Kabarebe

Pengine swala la Rujugiro linaharibu ushirikainao wa nchi hizi kwa kuwa Rwanda inamshataki kuwaunga mkono wapinzani wake ila Uganda humsaidia kuenedelea na shughuli zake za viwanda vya sigara,kaskazini mwake,jambo ambalo Uganda ilipinga kwa kusema kuwa wao hawahusishi uchumi na siasa.

Tajiri Ayabatwa Tribert Rujugiro

Taarifa hizi zinaeleza pia kuwa wanausalama wa Rwanda wanamshtaki waziri wa usalama nchini Uganda, (Rtd) Gen.Henry Tumukunde kuwa na urafiki wa dhati na Gen.Kayumba Nyamwasa na kuwa wanaongea kupitia simu.

Waziri wa usalama wa Uganda,Gen.Henry Tumukunde

Kuna taarifa kwamba  ndugu ye Rais Museveni,Gen.Salim Saleh anamtuma Tumukunde kukutana na Nyamwasa kule Afrika Kusini na kuwa Kayumba huja nchini Uganda kisiri kuwatembelea wanamgambo wa FDLR.

Mwenyekiti wa RNC,Gen.Kayumba Faustin Nyamwasa

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com