kwamamaza 7

Je,Rwanda haiamini Afrika kusini juu ya ushirikiano kati ya Waziri Maite Nkoana Mashabane na Jenerali Kayumba Nyamwasa?

0

Kuna taarifa kwamba Rwanda haiamini serikali ya Afrika kusini jambo linalowafanya wengi kujiuliza kama hili halitakuwa kuziuzi cha mabadiliko yanayotokea katika Umoja wa Afrika,UA kwa utawala wa Rais Paul Kagame.

Taarifa za Mail na Guardian zimeeleza Rwanda inadai kuwa kuna ushirikiano kati ya Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini,Maite Nkoana Mashabane na mwenyekiti pia kiongozi wa chama cha upinzani kwa serikali ya Rwanda,Rwanda National Congress(RNC ),Jenerali  Kayumba Faustin Nyamwasa.

Hizi taarifa zimekumbusha kuwa ushirikiano huu unazusha  kutoaminiana kati ya Rwanda na Afrika kusini kupitia Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini kwa sasa,Maite Nkoana Mashabane ambaye aliwahi kuwa balozi wa Afrika kusini nchini  Uhindi wakati ambapo Jenerali Kayumba Nyamwasa alikuwa balozi wa Rwanda nchini humo.

Waziri Maite Mashabane alipokuwa balozi nchini Uhindi//picha na Intaneti

Taarifa hizi zimeendela kueleza kwamba Waziri Maite ni rafiki wa dhati wa Rais Jacob zuma  na kuwa inatatanisha namna ambavyo Jenerali Kayumba Nyamwasa aliamua kukimbilia nchini Afrika kusini baada ya kukwepa kazi ya ubalozi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,watu karibu na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma walitangaza kuwa huyu hana furaha ya namna ambavyo Rais wa Rwanda,Paul Kagame anaongoza mabadiliko ya Umoja wa Afrika kwa kuwa anaona ni sawa na vile anavyoongoza Rwanda.

Kayumba Nyamwasa alikimbilia nchini Afrika kusini baada ya kuhukumiwa bila kuwepo kufungwa jela miaka 24 mwaka 2011 kwa juu ya mashtaka ya kuunda kundi la ugaidi,kuharibu usalama wa nchi ,uchonganishi na kukwepa kazi yake ya kijeshi.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.