Swahili
Home » Jen. Ngendahimana awashauri wanamgambo wa FDLR na chama cha Jen. Kayumba Nyamwasa
HABARI MPYA

Jen. Ngendahimana awashauri wanamgambo wa FDLR na chama cha Jen. Kayumba Nyamwasa

Jen. Jerome Ngendahimana,58, ambaye aliwahi kuwa mwanajeshi wa FDLR amewashauri  wanamgambo wa FDLR na chama cha Rwanda National Congress (RNC), cha Jen. Kayumba Nyamwasa kurudi nchini ili kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.

Jen. Ngendahimana kwenye hotuba yake baada ya jeshi la Rwanda (RDF)  kumpa pumziko, amewataka wanajeshi wa FDLR kutia silaha chini na kuja kuungana na raia wenzao kujenga nchi.

“ Ninatapa hii fursa kuwataka  wale ambao ni wanajeshi wa FDLR, RNC ambao wanajikaza kushambulia Rwanda kuacha  hiyo mipango kwa kuwa haitafaulu. Nawataka kuja kwa kujenga nchi yetu”

Ngendahimana ameshukuru jeshi la RDF lililomkaribisha bila kujali kuwa alikuwa  mwanajeshi wa jeshi ambalo ni “adui wa nchi”

“ Hawa ni wanajeshi waliokomboa nchi yetu, si jambo la kawaida nchi kumkaribisha adui wake kwa kuijenga nchi. Tunasimama mbele zenu kama ishara ya hiyo siasa nzuri ya umoja” amesema

Jerome Ngendahimana ni mwanajeshi wa cheo cha Jenerali. Alisajiriwa katika jeshi la utawala wa Meja Jen. Juvenal Habyarimana mwaka 1979. Alisomea shule la jeshi la ‘ Ecole Royale Militaire’ nchini Ubelgiji.

Alirejea nchini Rwanda mwaka 2003 kutoka nchini DR Congo.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com