kwamamaza 7

Jen. Kayihura alaani mashtaka ya kumteka nyara aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame

0

Aliyekuwa Mkuu wa Polisi nchini Uganda, Jen. Kale Kayihura amesimama kizimbani leo tarehe 24 Ogasti na kulaani mashtaka yote yakiwemo kumteka nyara na kumrudisha kwa nguvu  nchini Rwanda aliyekuwa mlinzi wa Rais Kagame, Luteni Joel Mutabazi.

Kwa mujibu wa taarifa za NTVJen. Kayihura anashtakiwa  mashtaka mengine yakiwemo matumizi ovyo ya silaha za Polisi tangu mwaka 2010 hadi 2018.

Jen. Kale Kayihura akiwa mahakamani

Luteni Joel Mutabazi alikamatwa na kurudishwa kwa nguvu nchini Rwanda mwaka 2013.

Alihukumiwa kufungwa maisha jela juu ya kuwa na hatia ya uhalifu wa kulenga kuharibu usalama wan chi kwa kuungana mkono na wanamgambo wa FDLR na RNC.

Watu wa karibu na Kayihura wanasema hana uhusiano wowote na hili kwa kuwa hili lilitekelezwa na akiwa ugenini.

Kwa  upande mwingine, Msemaji wa Polisi nchini Rwanda, CP Theos Badege alisema jambo hili lilifuata sheria za kimataifa.

Kesi ya Kayihura itaendelea tarehe 4 Septemba 2018

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.