kwamamaza 7

Jen. Kabarebe awalinganisha wapinzani wa Rwanda na nyuki wasiouma

0

Mshauri wa Rais Kagame kwa Mambo ya Jeshi na Usalama, Jen. Kabarebe amesema wapinzani wa serikali ya nchi yake ni  kama nyuki zisizouuma.

Jen. Kabarebe Jana  3 Aprili amesema wapinzani wa Rwanda kama vile Kayumba Nyamwasa, Callixte Sankara na FDLR si tishio kwa nchi hiyo kwa kuwa wana vurugu kati yao wenyewe.

Kuhusu Kayumba, Jen. Kabarebe amesema “  Kayumba ana vita vyake mwenyewe. Alichokosa katika hii safari ni mahitaji yake. Ilimkata kushika ha 1000 eneo la Umutara. Hilo ndilo lengo lake kurejea kutimiza hili.”

“Huyo Sankara simujui, ni kama mjanja kwa vijana mahali fulani. Niliwahi kusikia alikuwa hatari alipokuwa chuoni Butare mwaka 2009,” amefunguka kuhusu Sanakara aliyejigamba kushambulia kusini mwa nchi

Kwa ujumla kwa hawa wote, Jen. Kabarebe amesema “  Sijui wanacholenga, wanachowakilisha, hawawezi kua kitisho kwetu. Ni kama nyuki wanaokuwa kwenye sikio na hawawezi kudunga.”

Kabarebe amewahamasisha vijana waliokuwa katika mkutano mjini Kigali kuendelea kujenga nchi yao kwa kuwa wapinzani watabaki vile vile.

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.