kwamamaza 7

Jen.Kabarebe afunguka matusi ya Kanuni Lizinde baada ya RPA kukomboa uwanja wa ndege Kanombe

0

Waziri wa ulinzi Jenerali James Kabarebe ameweka hadharani alivyowatukana Kanuni Theoneste Lizinde wanajeshi wa RPA ( Rwanda Patriotic Army)  baada ya kukomboa   uwanja wa Ndege Kanombe mjini Kigali mwaka 1994.

Kwenye maadhimisho ya vijana waliouawa wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994 jana mjini Kigali, Kabarebe amesema Kanuni Lizinde aliwatukana wanajeshi wa RPA badala ya kuwashukuru kwani walimnusuru tarehe 21 Januari 1991 alipokuwa na wenzake gerezani mjini Ruhengeri.

“Wema huu haukumzuia Lizinde alipokuwa Byumba kupiga kelele kwa kusema”Watoto wa mbwa wameikomboa Kanombe?acha tungoje wanajeshi wa Bigogwe watawaonyesha”amesema

Kabarebe amekumbusha kuwa waliwanusuru pia Muvunanyambo,Biseruka na wengine na kuwapa vyeo vya juu katika jeshi kama ishara ya umoja.

“Tuliwanusuru na kuwapa vyeo katika jeshi letu kiasi wenzetu walikuwa wakiwaogopa.Hili likuwa ni ishara kwamba RPA ilikuwa inalenga umoja wa Wanyarwanda bila ubaguzi”

Waziri Kabarebe amewataka vijana kulinda yaliyotimizwa na kupiga marufuku jambo lolote linaloweza kurudisha Rwanda katika maovu.

Kanuni Lizinde alikuwa kiongozi wa Ofisi ya Upelelezi wakati wa uongozi wa Rais Juvenal Habyarimana.Baadaye  alifungwa jela kwa kutuhumiwa kuwaunga mkono Kanuni Alex Kanyarengwe aliyelenga kuipindua serikali ya Meja Jenerali Juvenal Habyarimana.

Kanuni Lizinde alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa nchini Kenya mwaka 1998.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.