kwamamaza 7

Je,mazungumzo ya siri  baina ya Rwanda na Ufaransa yatatoa suluhisho?

0

Wakati kunatarajiwa mazungumzo ya siri kati ya Rwanda na Ufaransa mjini Kigali,wengi wanajiuliza kama hili litatoa suluhisho la migogoro ya kisiasa iliyoko kati ya nchi hizi mbili tangu mwaka 1994.

Kinyume na haya,kuna matumaini kwamba nchi hizi mbili zitaweza kushirikiana kulingana na nia ya siasa iliyoko kati ya uongozi wa Rais Emmanuel Macron na Rais Kagame kinyume na marais wa zamani wa Ufaransa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

 Pia ziara ya viongozi wa wizara ya mambo ya njee Marechaux na Marie Edouard,mshauri katika ikulu ya Ufaransa mwezi wa Septemba walipozungumza na waziri wa mambo ya nje wa Rwanda,Louise Mushikiwabo ni dalili nzuri.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na hayo,inatarajiwa kuwa rais Kagame alialikwa katika  mkutano uliondaliwa na Ufaransa na Senegal mwezi Novemba 2017 kuhusu amani na usalama,kwa hiyo itakuwa fursa nzuri ya kukutana na Rais Emmanuel Macron ili kuzungumza kwa mapana na marefu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.