Waziri wa ulinzi,Jenereli James Kabarebe/Picha:Intaneti

Wengi wanajiuliza kama waziri wa wa ulinzi,Jenerali James Kabarebe ataenda nchini ufaransa kueleza mapana na marefu husika kuidungua ndege ya Rais Meja Jenerali Juvenal Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994.

Haya ni baada ya jaji,Jean-Marc Herbaut asili ya Ufaransa kumtumia Jenerali Kabarebe barua ya kuenda Paris tarehe 14 Disemba 2017 ili kuhojiwa mambo husika na kuidungua ndege aliyokuwemo Rais Habyarimana na Rais Cyprien Ntaryamira wa Burundi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa za RFI zinaeleza kuwa hili ni baada ya Ufaransa kusema kuwa kulionekana shahidi mpya,Frank Nziza ambaye alisema kuwa ni mmoja mwa waanajeshi wawili walioingia mjini Kigali wakibeba mabomu yaliyodungua ndege ya Rais Habyarimana.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,serikali ya Ufaransa hushataki jeshi la RPF kuidungua ndege ya Habyarimana,jambo ambalo serikali ya Rwanda hukana mno kwa kusema kuwa mashtaka haya ya kila mala ni kutaka kusahaulisha watu ushiriki wake katika mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Gaston Rwaka/Bwiza.com

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina