kwamamaza 7

Israel:Wakimbizi waamua kufungwa jela badala ya kuhamia nchini Rwanda ama Uganda

0

Wakimbizi asili ya Eritrea na Sudan nchini Isreael kwenye kambi ya Holot,jangwani Negevu wametangaza uamuzi wao kufungwa jela badala ya kuhamia nchini Rwanda ama Uganda kwa kusema kwamba hawawezi kuhamia nchini ambazo hawajui lolote kuhusu.

Mmoja wao kutoka Israel,Abda Ishmael,28 ametangazia AFP hawezi kuenda huko kulingana na yaliyowakabili wenzake waliohamia nchini Rwanda na Uganda.

Abda Ishmael amesema”Tuliona yaliyotokea kwa wale waliohamia nchini Rwanda na Uganda”.

Kambi ya wakimbizi ya Holot,jangwani Negevu

Huyu ameeleza kuwa alisikia maovu mengi yaliyowakabili wenzake, jambo lililowafanya wengi kuenda nchini Ulaya na kuuawa jangwani nchini Libya.

Mwenzake Shishay Tewelde, 24, ametangaza kwamba Rwanda na Uganda ni “nchi za kifo” na kusisitiza kuwa yeye ni tayari kufungwa jela la Sharonim,mahali ambapo watafungwa wakimbizi watakaogoma kuondoka Israel.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Raia wa Eritrea kwenye kambi ya ukimbizi wamesema kwamba Rwanda na Uganda hazina uwezo wa matarajio na kwa hiyo heli kufungwa jela nchini Israel kuliko kuhamia wasikokujua ili kutafuta ukimbizi.

Hata hivyo,Serikali ya Israel ilisema kuwa haina budi wakimbizi 1200 wa kambi ya Holot kuondoka nchini tarehe mosi Aprili 2018 na kuwa kinyume na hili watafungwa milele.

Takwimu za wizara ya mambo ya ndani ya Israel inaonyesha kuwa kuna wakimbizi 42,000 nchini Israel.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.