kwamamaza 7

Israel:Marubani wakataa kuwasafirisha wakimbizi nchini Rwanda na Uganda

0

Marubani wa kampuni ya El Al  kupitia mtandao ya kijamii wametangaza kutoshiriki katika kitendo cha serikali  cha kuwasafirisha wakimbizi 3800 nchini Rwanda na Uganda.

Kupitia Facebook, hawa marubani wamesema kwamba wameisha pokea wito 7500 wakishauriwa kutowasirisha wakimbizi mahali ambapo maisha yao yatakuwa hatarini.

Mmoja wao, Iddo Elad aliandika kwenye Facebook”Wasilisha wakimbizi kwenye kifo chao,nimeunga mkono wenzangu katika jambo hili na sitashiriki katika kisa hiki cha ushamba”

Mwenzake,Shaul Betzer juma pili aliandika kwenye facebook”Mimi rubani pia mwanadamu,haiwezekani mimi kushiriki katika kitendo cha kuwasilisha wakimbizi mahali ambapo maisha yao yatakuwa hatalini”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwingine Yoel Piterbag  aliandika  kwa kuwakumbusha Wayahudi kwamba nao waliwahi kuwa wakimbizi na hawakutaka watu kuwafukuza kama wafukuzavyo mbwa wa poli.

Taarifa za Timesofisrael zinaeleza kwamba waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu alisema kwamba hawa wanafrika siyo wakimbizi au wahamiaji  bali ni wahamiaji wa kiuchumi.

Isisahaulike kwamba Rwanda ilisema kwamba haikusaini mkataba wowote wa kuwakalibisha wakimbizi kutoka Israel,jambo sawa kwa serikali ya Uganda.

Bonyeza BWIZA TV kupata habari  na nyimbo mpya

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.