kwamamaza 7

Islam imeweka mikakati ya kupambana na itikadi kali na vitendo vya kigaidi ndani ya dini yake

0

Dini ya Islam ya Rwanda imetangaza, katika mkutanao na wanahabari Ijuma ya tarehe 16/6/2017 kwamba Islam imeiweka mikakati ya kupambana na mawazo ya itikadi kali ya kidini na hata vitendo vya kigaidi ambavyo vilijitokeza kwa baadhi ya waumini wa dini hiyo.

“Kuna teknolojia ya kupashana na kusambaza habari kwa haraka, hisia na mawazo ya itikadi kali ilisambazwa na njia ya teknolojia. Hadi sasa katika Rwanda kumejitokeza baadhi ya watu wenye mawazo hayo ya kuwa na kuunga mkono mawazo ya itikadi kali ya kidini hususani katika vijana wa dini ya Islam. Zaidi ya hayo, mojawapo wamefikia kiwango cha kushiriki katika makundi ya kigaidi aliyoko katika pande tofauti za dunia”Amesema, Sheikh Sindayigaya Musa, msemaji wa Shirika la waislamu nchini Rwanda.

Mojawapo wa vijana hao wanafutiliwa na mahakama kwa madai kama hayo. Na kulingana na hiyo shirika la waislamu la RMC limeweka mikakati ya kupambana na hiyo.

“RMC kama shirika lenye madhumuni ya kutangaza neno la mungu, kutetea, na kuimarisha dini ya islam. Imeweka mikakati ya kupampana na vitendo vilivyokuwa vimekwisha jitokeza”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baadhi ya mikakati hiyo ni kueka mwongozo maalum wa unabii na hata masomo yanayotolewa katika dini la Islam. Kwa hiyo hakuna mtu anayeruhusiwa kuja awe akitoka nchi za kigeni au popote nchi Rwanda kuingia mskiti au awajumuishe watu na aanze kuwafundisha kuhusu dini ya kiislam kabla hatujatambua kwanza asili na historia yake.

Inasemekana kuwa dini hili liliwapa mafunzo ya hali halisi ya suala hili viongozi wote wa ngazi za dini la Islam wakiwemo, waimam, wamufti, mashiekh, na dini liliunda mitaala na vifaa maalum vya kufundishia na kuwaelezea njama wanaotumia wenye kuhamisha vitendo vibaya kwa jina la dini ya Islam.

Vijana hawa kama kundi linalotumia teknolojia kwa wingi nao walipewa mafunzo Fulani.

Kuliwekwa pia miungano ya vijana katika wilaya zote ya kupambana na vitendo hivi nchini kote, na walijitolea lengo la kupambana na kuzuia vitendo na mawazo ya kigaidi miongoni mwa vijana.

Islam pia inashirikiana na idara za usalama kwa kupambana na kuzuia mawazo kama hayo kwa kupashana habari kwa wanaodaiwa uhusikaji.

Sindayigaya aliendelea kusema kuwa waliweka mikakati mingine kwa ajili ya kuboresha mbinu za kutoa misaada inayopewa watu wasiojiweza katika mwezi Ramadhan, kitendo ambacho baadhi ya watu wangetumia kutekeleza vitendo vyao visivyolingana na imani ya Islam.

Sheikh huyu alisisitiza pia kwamba haimo kuua ama kushiriki ugaidi katika kanuni za kiislam.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.