Home HABARI MPYA Ingabire Marie Immaculée Yalinganisha kufungwa kwa vyuo na kutokuwa na utawala bora
HABARI MPYA - SIASA - June 24, 2017

Ingabire Marie Immaculée Yalinganisha kufungwa kwa vyuo na kutokuwa na utawala bora

Ni katika kipindi cha redio Rwanda kulipokuwa kukizungumzwa mambo mbalimbali yakiwemo ya utawala bora na hata matatizo yaliyomo katika sera za serikali.

Kiongozi huu wa shirika la Transparency International Rwanda ya kupambana na uonevu na hata rushwa amegusia masuala mengi yanayojitokeza kwa baadhi ya viongozi mbali mbali na ni pingamizi dhidi ya haki za raia. Huku aligusia kesi za mahakama zinazoamriwa kwa kuegamia upande fulani na kufanya watu kukata rufaa kwa mpatanishi wa serikali(ombudsman) na kupendeza zipunguke.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“ Ningependa kuomba tatizo za kesi zinazopelekwa kwa mpatanishi wa serikali zipunguzwe kwa angalau kwa nusu” Asema Alihusisha hili hususani na kuwepo kwa rushwa. Akigusia kuhusu vyuo vilivyofungwa alisema kuwa hii inaweza ikahusishwa na kutokuwepo kwa utawala bora kwa kuwa kauli hii ni ya kuathiri wazazi na hata vyuo pekee yake.

“ni aibu sana viongozi wanatoa ruhusa kwa vyuo kuanza masomo na mara tu katikati mwa mwaka wakatoa kauli ya kusitisha masomo yao, hiyo huathiri watu hususani wasio na uhusikaji wowote namjua mzazi aliyeuza kipande cha shamba lake kwa ajiri ya karo ya chuo na kwa hivi mtoto anakaa nyumbani baada ya chuo chake kuamriwa kusitisha masomo”

Akiulizwa mtazomo wake juu ya suala hilo amesema

“ wanaostahili kulaumiwa ni wale waliotoa vyeti vya kuwaruhusiwa kuanzisha masomo bali si wazazi na watoto sasa ungemwambia mtuu hiyo ni aina gani ya Utawala bora?”

Jopo lililokuwa katika mzunguzo katika kipindi hicho limependekeza mabadiliko katika awamu ya miaka 7 mbele.

Uamuzi wa kuvifunga na kushurutisha vyuo kufunga idara mojawapo za masomo ulichukuliwa na wizara ya elimu na imelezewa ni kwa madhumuni ya kupigania elimu bora ya vyuo.

Vyuo vilivyofungiwa milango ni pamoja na Rusizi International University, Chuo cha Gitwe(baadhi ya masomo) ,Mahatma Gandhi University na vinginevyo.

Mpaka sasa wakufunzi wa vyuo hivyo hawajuwi hatima ya hiyi kauli huku wakingojea ikiwa serikali italegeza na kuwaacha wakaendelea masomo. Aidha Baraza la Elimu ya vyuo vikuu iliwaahidi kwamba wakufunzi ambao wanataka kuendelea na masomo yao itawasaidia kupata usajili katika vyuo mpya.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.