Mvua ilionyesha jana Ijuma tarehe 3 Mach 2017 ilibomoa nyumba za watu wengi, kaharibu mavuno shambani, mafugo kauawa, biashara kaharibika na mambo mengine ya msingi katika wilaya ya Rubavu na Nyabihu jimbo la Mangharibi na wilaya ya Ngoma jimbo la Mashariki.

Mvua ilionyesha katika wilaya ya Rubavu na Nyabihu ilikuwemo upepo mwingi na ilivuma kutoka katika mlima wa mstu Gishwati jana jioni na kuharibu mambo mengi pakiwemo nyumba za raia, shule, makanisa na mavuno katika tarafa ya Bigogwe wilaya Nyabihu, na tarafa ya Kanzenze wilaya ya Rubavu.

Kiongozi wa tarafa ya Kanzenze Uwimana Monique, alisema ya kuwa upepo ulivuma sana katika kiini ya Nyamikongi na Renga.

Kiongozi wa wilaya ya Rubavu mwakilishi anayehusika na uchumi Murenzi Janvier alisema ya kuwa wanaendelea kufanya orodha ya mambo yalio haribika, na pia alisema ya kwamba walio fikiwa na dharura, wilaya itabaki karibu nao katika mabo yote.

Hata kama wanaendelea na kufanya orodha wanasema ya kuwa nyumba zilizobomoka ni zaidi ya 40 na raia wawili wakajeruhiwa.

Katika wilaya ya Ngoma, mvua iliharibu mambo ya biashara katika soko kubwa ya wilaya katika tarafa ya Kibungo, mbuzi 6 zikafariki katika tarafa ya Rukira katika wilaya hio, katika wilaya hio pia nyumba za raia zilibomoka.

Rwiririza Jean Marie Vianney, kiongozi wa wilaya ya Ngoma mwakilishi anayehusika na uchumi alisema ya kuwa wameanza kufanya orodha ya mambo yalio haribika kwa ujumla.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

Leki@bwiza.com, chanzo:imvaho

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.