kwamamaza 7

IMF yasifu uchumi wa Rwanda

0

Shirika la fedha la kimataifa, IMF linasifu hali ya kiuchumi ya nchi ya Rwanda ijapokuwa nchi hii inaweza kukabilwa na kushuka kwa thamani kutokana na ughali wa mali na vyakula.

Uchumi ulishuka duniani katika mwaka wa 2016, lakini Rwanda ilibaki na kiwango cha 6% cha ongezeko la uchumi katika mwaka uliopita.

Mtumishi wa IMF,  Laure Redifer aliyezuru Rwanda ili kuchunguza hali ya mambo ya uchumi; alithibitisha kwamba hali ya kiuchumi ya Rwanda inakuwa thabiti kulingana na nchi nyingine zinazokuepo chini ya jangwa la Sahara.

[ad id=”72″]

“Lengo la kuongeza uchumi nchini rwanda ingali 6%, ni kiwango cha juu kulingana na nchi nyingine chini ya jangwa la Sahara. Tulifikilia kwamba uchumi wa Rwanda ungeshuka kwa ajili ya jua kali lililotokomeza mimea na kuleta ukame,” Laure Redifer alisema.

Waziri wa fedha na mipango ya uchumi, Claver Gatete alisema kwamba kulingana na hali ya sasa; uchumi hautashuka chini ya kiwango cha 6%. “Baada ya kuchunguza hali ya uchumi na nguzo za uchumi mithili ya viwanda, huduma na ukulima; tulisadiki kwamba uchumi wetu hautashuka.”

[ad id=”72″]

Mwanzoni mwa 2016, nchi ya Rwanda iliapa kuongeza uchumi kwa kiwango cha 6%.

Mnamo mwezi Juni, shirika la IMF lilipatia Rwanda mkopo wa fedha milioni 2014 za dola la Marekani ili kuimarisha sekta mbali mbali za uchumi hasa hasa ukulima.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.