kwamamaza 7

Ilivyokuwa katika kampeni za Paul Kagame wilaya ya Burera na Gakenke

0

Kampeni za siku ya leo tarehe 31 za mgombea wa chama cha RPF zimefanyika katika wilaya ya Burera na hatimaye Gakenke.

Kwenye uwanja wa Birambo palipokuwa pamejumuika maelfu ya wananchi kadhaa, alipofika hapo Rais Kagame alianza kuwasalimu kwa kuwapepea na raia hao wakamjibu kwa shangwe.

Hapa wananchi kupitia aliyetoa ushahidi walimuahidi rais Kagame kwamba watampa kura zao kwa uwingi.

Katika hotuba yake alianza kwa kuwaelezea kwamba kumchagua mgombea wa RPF Ni kuchagua mema, siasa inayofaa, kuendelea kujenga miundmbinu na shughuli nyingine nyingi za maendeleo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wananchi

“ hapa Burera na hata sehemu zinazopakana, tulipaishi,tukapapigania vita, na kuvishinda, hatua ya sasa ni kupajenga upya, tunachotaka ni kujiendeleza, yote yanawezekana, yalitokea kuwezekana, na yatawezekana bila shaka kwa sababu yenu, kwa sababu ya ushirikiano wenu, na kukiwa na siasa nzuri hakuna sababu yoyote Burera itakosa kuendelea” amesema . Aliendelea kuwaahidi kwamba yote yatawezekana kwa sababu kuna ushiriano madhubuti kati ya wanyarwanda ikiongezeka siasa nzuri.

Alivishkuru pia vyama nane vilivyojiunga na RPF na kumwunga mkono mgombea wake katika uchaguzi wa hapo mwezi Agosti.

Mweneyekiti wa PSD Jean Damascene Ntawukuriryayo

Amewahimiza kumaliza kazi mapema tarehe 4 Agosti na kwamba atarudi kuwashkuru baada ya uchaguzi.

Alipomaliza hapo aliendelea na shughuli zake wilaya ya Gakenke

 Alianza kwa kusema kwamba mabadiliko yaliyofikiwa katika utawala wa RPF ni ya mema yasiyo na kiwango.

“na hata tunapofanya kampeni za kusaka kura hatusemi uongo tunasema mambo yaliyo halisi, yaliyofanyiwa ni ukweli usio kuongeza chumvi, hatuwezi kuja hapa mbele yenu na kuwaahidi ambayo hatuataweza kuyafikia.”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Amewahimiza raia hao kuwa na ari ya kufanyakazi kwa kushirikiana na kufanya kazi kama wafanyakazi binafsi na hata kwa kushirikiana.

Wanachama wa PL

Aliendelea kuwaonyesha mifano halisi ya historia mbaya ambayo Rwanda iliipitia na kuwaambia kwamba huyu ni wakati mwafaka wa kuiachia nyuma na kuanza na historia mpya ya kuijenga nchi na kujiendeleza kufuata mfumo huwo wa kihistoria ulioletwa na utawala wa RPF.

Aliendelea kwa kuwahimiza kupambania maendeleo yasiyomwacha nyuma yeyote, vijana wanasoma moja kwa moja kwa kujitafutia kazi, kuendeleza siasa ya kijinsia na hata kuwa na desturi  ya kupambania kujiendeleza.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.