kwamamaza 7

Ikulu ya Rwanda yakana taarifa za kukutana kati ya Rais Kagame na Rais Museveni

0

Ikulu ya Rwanda kupitia kiongozi wa wajibu wa mawasiliano,Yolande Makolo imekana taarifa za vyombo vya habari nchini Uganda zisemazo kuwa  Rais wa Rwanda,Paul Kagame alikutana na kuzungumza na Rais wa Uganda Yoweli Kaguta Museveni mjini Dubai walipohudhuria katika mkutano wa ‘Global Business’ wiki iliyopita.

Taarifa zilikuwa zikisema kuwa viongozi hawa wawili walizungumza kuhusu namna za kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo ya eneo la Afrika mashariki.

Pia,waziri wa mambo ya nje wa Uganda,Okello Oryem alionekana katika taarifa hizi akisema kuwa Rais Kagame na Rais Museveni walikutana  nchini Umoja wa falme za kiarabu na kuwa umoja wa nchi hizi mbili ni mzuri.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande wa Rwanda,Yolande Makolo aliyekuwa pamoja na Rais Kagame mjini Dubai ametangazia Chimpreports kuwa hajui lolote kuhusu mkutano huu mjini.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Pamoja na haya,Chombo ambacho hakikutajwa jina kilijaribu kuwaomba mafisa wa mambo ya nje thibitisho la kuwa Rais Kagame alikutana na Rais Museveni kama vile picha ama video wakagoma.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri Oryem kupitia simu alisema kuwa viongozi hawa walikutania ukumbini wa mkutano,wakasalimiana na kuongeza kuwa hii ni ishara ya kuwa ushirikiano kati ya nchi hizi ni mzuri sana.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya taarifa za chimpreports za wiki iliyopita kueleza kwamba kuna vita baridi kati ya nchi hizi juu ya ulinzi,kuwateka nyara  wakimbizi,upelelezi na kutotimiza ahadi za miradi ya maendeleo kati ya nchi hizi na kadhalika.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.