kwamamaza 7

ICGLR  yataka mashirika ya kimataifa kutoa suluhisho kwa masuala ya Rwanda na Burundi

0

Shilika la Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) imetaka Umoja wa Afurika (UA0 na Umoja wa Kimataifa (YUNA) kutoa suluhisho kwa masuala ya ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi.

Katibu Mtendaji wa  ICGLR, Zachary Muburi-Muita, ametangaza hayo kwenye mkutano wa hili shilika kuhusu usalama katika nchi za maziwa makuu.

Huyu mwanadipolomasia amesema ushirikiano ovyo kati ya Rwanda na Burundi ni jambo linalohangayikisha ICGLR na kutaka UA na YUNA kutoa suluhisho.

Muburi- Muita amesisitiza hili linastahili kupata suluhisho kwa kuwa uwepo wake unaathiri shuguli nyingine za shilika la  ICGLR.

Mwakilishi wa YUNA kwenye maziwa makuu, Said Djinnit  amesema alikutana na Kiongozi wa ICGLR, Denis Sassou Nguesso ila mikakati yote waliyoanzisha haikufua dafu.

[penci_related_posts taxonomies=”undefined” title=”Habari nyingine” background=”” border=”” thumbright=”no” number=”4″ style=”list” align=”none” displayby=”recent_posts” orderby=”random”]

Kwa mujibu wa taarifa za Iwacu Burundi, Djinnit ametia msisitizo suala la Rwanda na Burundi linastahili kuungana mkono kwa kutafuta suluhisho.

Ushirikiano kati ya Rwanda na Burundi ulianza kuwa ovyo tangu mwaka 2015.Burundi ilishtaki  Rwanda kuwaunga mkono waliolenga kupindua utawala wa Rais Pierre Nkurunziza.

Rwanda ilikanusha haya madai kwa kusema haina faida yoyote kwa kujihusisha na vurugu la kisiasa nchini Burundi.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.