kwamamaza 7

Huye:Wafanyabiashara watangaza uhaba wa wateja kufuatia uhamishaji wa wanafunzi wa chuo

0

Baadhi ya wafanyabiashara katika wilaya ya Huye wametangaza kupungua kwa wateja na kufanya biashara yao kuyumba kufuatia kundi kubwa la wateja wao kuhamishwa.

Wafanya biashara kwenye maeneo yanayopakana na chuo kikuu cha UR-Huye wanasema kuwa asilimia kubwa ya wateja wao ni wanafunzi wa chuo kikuu na kwamba tayari kuna wafanya biashara wenzao waliokomesha shughuli zao kufuatia hali hiyo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mmohja wao David Tumushime ambaye ni mmiliki wa duka la vifaa vya elimu anaelezea kuwa  biashara yake inakwenda vizuri ingawa sivyo kama ilivyokuwa hapo awali. “Mimi sioni sababu ya kukata tamaa,ikiwa nafanya bishara yangu na kuweza kupata kipato ambacho kinaniwezesha kulipa nyumba,nakula na hata naweka fedha kwenye benki.”

Pia David amesema kuwa changamoto kubwa ni pale wanafunzi wanapokwenda likizo.Shughuli zake husimama kwa miezi zaidi ya miwili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katibu mkuu mtendaji wilaya ya Huye, Vedaste Nshimiyimana, amekanusha habari hizo na kwamba sio kweli kwamba wanafunzi waliohamishwa walikuwa na mchango mkubwa na mendeleo ya biashara katika wilaya Huye.

Bw Vedaste ameleza kuwa biashara zipo za aina nyingi na kwamba kuna mafunzo kadhaa yanatolewa kwa wafanyabishara wadogo wadogo katika kuendeleza shughuli zao,na hivyo matumaini makubwa yapo kwani hadi sasa wameshatoa mafunzo kuhusu shughuli hizo wakishirikiana na wizara ya kazi,wizara ya biashara,SACCO,na pia WDA.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wafanya biashara kadhaa ambao hawakutaka majina yao yatajwe hususa maeneo ya karibu na chuo kikuu,soko jipya sehemu ya matunda,nguo za mitumba na hata wenye bishara za mama ntilie ,wamelalamika wakisema kuwa hali sio nzuri kama ilivyokuwa hapo awali.

Hali hiyo inafuatia idadi kubwa ya wanafunzi waliohamishwa kutoka chuo kikuu cha taifa UR-Huye, baada ya vitengo vyao kupelekwa katika vyuo husika.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Hassan Thabiti/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.