kwamamaza 7

Hotuba kali za rais Kagame zilizoashiria katika  mwaka wa 2016

0

Tangu sikukuu ya kufungua mwaka huu tarehe 1Januari 2016 hadi Oktoba, mwaka wa 2016 unakosa miezi miwili kumalizika. Kuna hotuba kali zilitolewa na rais Kagame na kuchukuliwa kuwa maalum kwa raia wa Rwanda; mfano wa hotuba ya rais Paul Kagame ya kuanzia mwaka wakati alipothibitisha kugombea urais.

Baada ya kura ya maoni (Referandum) ilifanywa kwa maombi ya raia na kutihibitishwa bungeni kuhusu vipindi vya rais, kura takribani 98% zilimkubalia rais Kagame kugombea urais baada ya 2017; ijapokuwa yeye alikuwa bado kutangaza msimamo wake.

Hotuba ya kufungua mwaka tarehe 1 Januari 2016, rais Kagame alisema; “Cha kwanza nawatakia mwaka mpya mzuri wa 2016, utakuwa wa mambo mazuri na maendeleo;…Mliniomba kuendelea kuongoza nchi baada ya 2017, kulingana na uzito wa maombi hayo; siwezi kukataa. Kinachobaki ni kufuatilia mwendo sawa wakati ambapo muda utafika”.

[ad id=”72″]

Hotuba nyingine kali ya rais Paul Kagame, ni wakati alipojibu nchi ya Burundi baada ya maandamano ya raia na viongozi wa Burundi ya kusumbua nchi ya Rwanda. Kagame alisema, “Nilisikia maneno kwamba watatufunyanga, lakini nao wanajua, wanajua kwamba hawawezi kupita msitari usiopitwa.”

Wakati wa kuanzisha mwaka wa mahakama bungeni, rais Kagame alitoa hotuba kali juu ya nchi ya Ufaransa baada ya wanasheria wa nchi hii kuamua tena uchunguzi kuhusu kifo cha rais wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyariama.

[ad id=”72″]

Kagame alisema kwamba mabalozi wa Ufaransa wanaweza kukimbizwa nchini Rwanda. Alisema, “Kama kurudia uchunguzi huu ina maana ya kupingana; tumejitaarisha kupingana hakuna shida.”

Hotuba za rais Kagame zilichukuliwa vizuri na raia kwani zilitoa msimamo wa nchi juu ya kesi mbali mbali hasa hasa juu ya nchi za kigeni. Mfano wa maoni ya wananchi juu ya hotuba za rais, ni wakati alipokuwa na wanafunzi wa vyuo vikuu; alipigiwa makofi baada ya kuonya Burundi kutoingilia uhuru wa Rwanda.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.