Home HABARI Hatutatuma waangalizi nje ya Nairobi-Umoja wa Ulaya
HABARI - KIMATAIFA - October 25, 2017

Hatutatuma waangalizi nje ya Nairobi-Umoja wa Ulaya

Waangalizi wa Kimataifa wanaofuatilia Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi nchini Kenya, wametangaza kutotuma waangalizi wake katika Kaunti mbalimbali nchini humo.

Viongozi wa waangalizi hao kutoka Umoja wa Ulaya,Jumuiya ya Madola na Taasisi ya Carter, wamesema wamechukua hatua hii kwa sababu za kiusalama.

Hata hivyo, waangalizi hao wamesema watasalia jijini Nairobi kuangalia namna matokeo yatakavyokuwa yanatumwa katika kituo cha kutangazia matokeo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hata hvyo, waangalizi wengine kutoka Umoja wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Afrika Mashariki, hawajazungumzia lolote kuhusu wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama nchini humo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Umoja wa Afrika una waangalizi 100, waliotumwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wito wa waangalizi hao kuhimiza mazungumzo kati ya wanasiasa nchini humo haujafua dafu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Asili:rfi

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.