kwamamaza 7

Hata walevi, wazinzi, wachawi na waongo wanaimba nyimbo za kuabudu Mungu

0

Bwana Yesu asifiwe: Zaburi 96:9″Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu, tetemekeni mbele zake, nchi yote”.
Msingi wa wokovu uko katika kumwabudu Mungu.Na kuabudu siyo kuimba nyimbo za kuabudu kwa taratibu maana hata walevi, wazinzi, wachawi na waongo wanaimba nyimbo za taratibu.
Lakini sura halisi ya kuabudu ni mazingira ya MAISHA MATAKATIFU tunayoishi siku zote, haijalishi uko kanisa au hauko kanisani, maandiko yatwambia…”MUNGU NI ROHO, NAO WAMWABUDUO YEYE IMEWAPASA KUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI”.

Kwa maneno hayo tuna uhusiano wa roho yako ndiyo chanzo cha KUABUDU KWA UZURI NA UTAKATIFU. Na kweli iliyo Neno la Mungu inakuweka huru mbali na dhambi.
Ndiyo maana tunaambiwa..”Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa na” Waebrania 12:14.
“MAISHA MATAKATIFU YAKO NDANI YA YESU”.
Yohana 1:4″Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, na ule uzima ulikuwa nuru ya watu”
Yohana 8:12″Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hata kwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima”
Angalia lile Neno “NURU YA UZIMA” Maana yake ni “MAISHA YALIYO JAA MWANGA” ndiyo maana maandiko yanatwambia,,”Ninyi ni nuru ya ulimwengu” kama wewe ni nuru maana yake maisha yako ya UTAKATIFU yanahitajika yawaangazie walio gizani ili wauone uzima ulioubeba ndani yako.
Ukikaa ndani ya Yesu unabeba UZIMA uliyo ndani yake, na huo uzima utakuwa nuru kwa watu wengine….Paulo anasema”Si mimi ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu”
Yesu akiishi ndani yako lazima matendo yako yabadirike kuanzia USEMI, UVAAJI, NA MWENENDO WOTE.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.