kwamamaza 7

Harusi ya kushangaza ya bi harusi wa miaka 5 na mvulana wa miaka 22

0

Polisi wa mijini Dhakan nchini Pakistan yasitisha harusi ya kisichana chenye umri wa miaka mitano na kuwakamata watu ambao walikuwa wakishiriki harusi hiyo.

Inasemeka familia ya msichana huyu mchanga imeamua kumtoa mtoto wao kwa kuwa wamekuwa wakilenga kupata maslahi ya mali. Walimvalisha mavazi ya harusi na wakawaalika wanafamilia hizo mbili na hata mtu aliyekuwa akijitolea kuwafungisha ndoa mvulana huyo na kisichana.

Polisi imesema  imefika baada ya sherehe kukamilika ila imewahi kumkamata Habibullah Shar aliyejifanya bwana harusi, wazazi wa mtoto akiwemo babake Gul Meer na Molvi Kifayatullah Bhutto ambaye amekuwa akitaka kuwafungisha ndoa.

Polisi ya nchi ya Pakistan imelaani tendo hili kwa kusema ni unyanyasaji usio wakusamehewa na kuwa umefanyiwa hadharani bila kuwepo yeyote kuupinga kama vile ni harusi kwa msichana mzima.

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kwa sasa amewahudumia kisichana kile na mamake vile vile kwa kuendesha uchunguzi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.