Home HABARI MPYA Hali ni mbali utawala wa Kabila ukifikia mwisho
HABARI MPYA - December 19, 2016

Hali ni mbali utawala wa Kabila ukifikia mwisho

[ad id=”72″]

Hali ya kisiasa nchini Congo-Kinshasa na mgomo ukitokota wakati muhula wa pili wa rais Kabila unafikia mwisho leo tarehe 19 Disemba 2016

Maongezi ya suluhisho kati ya upinzani na serikali ilifanyika juma nenda na hawakutatua lolote, na mazungumuzo yametayarishwa na kuongozwa na viongozi wa Kanisa kalotika itafanyiwa tena tarehe 21 Disemba.

Hofu ni kubwa watu wakizania huenda kutakuwa mgogoro nchini DRC kwa ajili ya kupinga kwamba rais Kabila aweza bania utawala kwa njia isio halali.

[ad id=”72″]

Pia upinzani husema kwamba Rais Kabila ndie alizua mzozo kwa kutafuta kuwania uongozi, mwezi Septemba watu zaidi ya 50 waliuawa kwenye maandamano ya upinzani, na maafisa 3 wa polisi walifariki kwenye mzozo huo.

Rais Kabila asema atabaki madarakani kwani uchaguzi haukufanyia kama vile ilitayarijiwa mwezi Novemba na hakuna mtu wa kukamata na fasi ya uraisi, na uchaguzi umehamishwa hadi mwaka wa 2018.

Waziri wa mawasiliano Lambert Mende asema: “Kabila atasalia madarakani hadi rais mpya achaguliwe. Hakuna jambo jingine litakalofanyika. Mtu akijaribu kuvuruga amani hapa mjini, atakumbana na polisi kama inavyofanyika maeneo mengine duniani”.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com, chanzo bbc-kiswahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.