kwamamaza 7

Hakuna mtu mwenye hekima atakayenunua jengo langu-tajiri Rujugiro

0

Tajiri Ayabatwa Tribert Rujugiro leo ameweka wazi kwamba mtu mwenye akili hawezi kununua jengo lake la kifahari kwa jina la Union Trade Center (UTC)linalotarajiwa kuuzwa kwa mnada akijua vikwazo vilivyomo.

Jengo la UTC litakalouzwa kwa mnada

Tajiri huyu kupitia radiyo sauti ya marekani amehoji haya baada ya Ofisi kuu ya nchi ya ushuru (RURA) kuweka hadharani tangazo likieleza kuwa jengo lake itauzwa kwa mnada baada ya kutolipiwa ushuru kiasi frw biliyoni moja na miliyoni 100 kuanzia mwaka 2007 hadi 2013.

Tangazo la mnada kwa jengo la UTC lililotolewa na RURA

Madai haya ameyakana Rujugiro kwa kufafanua kwamba jengo lake lilichukuliwa mwaka 2013 na kuwa lilikuwa likimpatia $miliyoni 1.5 kila mwaka na kuwa sheria inaeleza kuwa 50% za jengo hili zinapatiwa mali hii wakati wa miaka minne.

Jengo langu lilipatiwa miliyoni $ miliyoni 2.5, wananiomba ushuru wa $ miliyoni 1.2, kwa nini hawatumii hizo kwa kujilipa ushuru?” amesema tajiri Rujugiro.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rujugiro ameongeza kuwa hatakubali kulipa ushuru wakati wa siku 15 na kusisitiza kwamba mchezo huu wa kuigiza wa ushuru ni ujanja wa serikali wa kumunyanganya jengo lake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rujugiro alijulikana kuhusu shughuli za viwanda vya sigara na kuwa mshauri wa Rais Paul Kagame kuhusu mambo ya uchumi lakini siku hizi alikimbia nchi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.