kwamamaza 7

Habari zilizostajaabisha barani Afrika mwaka 2017

0

Matukio mengi ya kukumbukwa yalitokea mwaka 2017 yakiwemo kujiuzulu kwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mabadiliko sambamba katika nchi za Gambia na Angola.

Isisahaulike kufutwa kwa uchaguzi wa rais nchini Kenya ,kitendo kilichofanyika kwa mara ya kwanza Afrika.

Pia tumeripoti kuhusu majanga na ubunifu – lakini hizi ni baadhi ya habari za kushangaza kwa mwaka 2017.

‘Githeri Man’

Mwanaume mmoja Mkenya aliyepigwa picha akitafuna ‘githeri’ chakula cha mahindi na maharagwe, wakati wa uchaguzi, alijipatia umaarufu mkubwa.

Githeriman, ambaye kwa jina lake halisi anaitwa Martin Kamotho, alivuma wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya tarehe nane mwezi wa nane alipoonekana kwenye mitandao ya kijamii akila chakula cha maharagwe na mahindi yakiwa ndani ya mfuko wake wa plastiki.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Bw Kamotho anajulikana sana kama “Githeri Man” alivuma sana kwenye mitandao ya jamii.

Kanisa la Walevi

Kanisa jipya nchini Afrika ya Kusini lilifungua milango yao na kuwakaribisha wavuta sigara na wanywaji pombe , ambao kwa kawaida hawapatiwi nafasi katika makanisa ya walokole.

Mtandao wa Habari Afrika Kusini ya eNCA, iliripoti kuwa, kanisa la Gobola mjini Johannesburg liliwakaribisha makundi ya watu na chupa za bia wakati wa ibada.

Wabunge watwangana makonde Uganda

Wabunge nchini Uganda walipigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wabunge wa upinzani wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa ni njama za kumuandilia njia Rais Yowei Museveni, mwenye miaka 73, kugombea tena mwaka 2021.

Katika kanuni za Katiba, mtu anayewania urais haruhusiwi kuwa na umri zaidi ya miaka 75.

Suruali ni Marufuku Sudan

Polisi nchini Sudan walivamia sherehe katika mji mkuu wa Khartoum mwezi Disemba na kuwakuta wanawake wakivaa suruali.

Wanawake 24 walikamatwa na kushtakiwa kwa kutokuwa na maadili lakini baadaye mashtaka hayo yalifutwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Shambulio hiyo ilifanywa na idara ya poilisi yenye mamlaka ya kulinda maadili.

Kama wanawake hao wangehukumiwa, wangepata adhabu ya mijeledi 40 na kutozwa faini.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wanakamtwa na kupigwa kwa “kuvaa nguo zisizo na maadili” kila mwaka na kuichapwa mijeledi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wanasema sheria inayopiga marufuku kuvaa suruali, sketi fupi au ya kubana katika nchi ambayo wengi ni Waislamu, ni ubaguzi dhidi ya Wakristo.

Kitamaduni, wanawake wa Sudan wanavaa nguo ndefu zisizobana kama baibui.

Asili:BBC

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.