kwamamaza 7

Gundua tarehe ambayo Rais Kagame atakula Kiapo baada ya kushinda uchaguzi

0

Rais Kagame ambaye alitangazwa na tume ya uchaguzi kwamba ndiye mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 4 Agosti kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 98 atakula kiapo wiki ijayo.

Siku yenyewe ambayo rais huo atakusimama kizimbani akila kiapo cha kuongoza Rwanda kwa muhula wa tatu wa kipindi cha miaka saba, itakuwa   Ijumaa Tarehe tarehe 18 mwezi huu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katika shughuli hii ambayo itafanyika uwanja wa Amahoro, kutakuweko wageni na wanasiasa wa vyeo na hata wakuu wa nchi za kigeni.

Shughuli ya kuapishwa kwa Rais Kagame itapeperushwa kwenye vituo vya televisheni na redio vya taifa na wananchi wataweza kuifuata wakiwa kwenye vijiji vyao. Kuna habari nyingine zisemazo kwamba kutakuwa na mastaa waimbaji ambao watakuwa wakiwaburudisha wanyarwanda kwenye wilaya mbalimbali za nchi.

Rais Kagame ambaye alitangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa rais kwa asilimia zaidi ya 98 ataiongoza Rwanda kwa muhula wa tatu aliowania baada ya mabadiliko ya katiba yaliyokuweko kufuatia kura ya maoni iliyombwa na mamilioni ya wanyarwanda kwa kuasirisha nyaraka zao kwa tume ya Uchaguzi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.