kwamamaza 7

Gisozi: Mfalme Mohammed VI azuru kituo cha kumbukumbu

0

Mfalme wa nchi ya Morocco inayopatikana kaskazini mwa Africa Mohammed VI, katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Rwanda; alikizuru kituo cha kumbukumbu juu ya mauaji ya kimbari Gisozi na kutia maua kwenye kaburi za waathirika wa mauaji ya kimbari ya watutsi mnamo 1994.

Alipazuru jana 20 Oktoba 2016 pamoja na waziri wa maliasili Dkt Vincent Biruta na waziri wa utamaduni na michezo Julienne Uwacu na viongozi wengine.

[ad id=”72″]

Baada ya kutia maua kwenye kaburi za waathirika zaidi ya 250,000; alisafirishwa ndani ya nyumba zinazohifadhi historia kuhusu mauaji ya kimbari, maandalizi ya mauaji ya kimbari, utekelezaji wa mauaji ya kimbari na jinsi ilikomeshwa.

mfalme wa Morocco
Mfalme Mohammed alielezewa historia ya mauaji ya kimbari

Uongozi wa kituo cha kumbukumbu cha Gisozi umetangaza kwamba mfalme Mohammed VI aliaacha ujumbe wa kuhamasisha raia wa Rwanda juu ya umoja.

[ad id=”72″]

“Mauaji ya kimbari ni wakati wa giza katika historia ya wanyarwanda wote. Ni hali ngumu kwa binadamu. Leo Rwanda inapata nafuu na kurudi maishani, ni matumaini ya leo na kesho; tunaamini kwamba kesho kutakuwa na muungano, umoja, usalama,” Ujumbe ulisema.

Honore Gatera ambaye ni kiongozi wa kituo cha kumbukumbu cha Gisozi alisema kwamba ziara ya mfalme Mohammed VI itasaidia kufundisha dunia nzima mauaji ya kimbari ya watutsi na kupambana na mauaji haya kurudiwa popote duniani.

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.