kwamamaza 7

Gishari: Hata kama viongozi wanakana uwepo wa viboko raia wanaomboleza

0

Katika kijiji Ruyenzi, tarafa ya Gishari, kuna jamii zaidi ya 35 wakihusika na ukulima kama viyazi sukari, mihogo, mutama, mahaindi na mengine ila wanalima kando ya ziwa Muhazi kwa kiwango ya meta 50 kama vile husema sheria.

Raia hao wanaomboleza kwa sababu mavuno yao yanaharibiwa na viboko wanao toka katika ziwa Muhazi, wanasema kuwa hawajui wataishi kwa nini sababu wanakosa waulize wapi swala hilo la wanyama wanao haribu mavuno yao.

Wakaaji waliendelea na kusema kwamba wanyama hao kwa usiku wanakula mimea na nafasi wanakanyaga hakuna mavuno kwa kuwa ni uharibifu mtupu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kinacho sikitisha raia ni kwa sababu wanakosa waende wapi, anaye husika na usalama katika kijiji anahakikisha kwamba viboko wanaharibu mimea, alijaribu kujulisha ngazi kama uongozi wa kijiji na uongozi wa kiini ila hakuna jibu kwa hayo.

Kiongozi wa tarafa ya Gishari yeye anasema ya kuwa katika ziwa la Muhazi hakuna viboko kwa muda wa miaka 20 hawaonekani tena.

Uongozi wa wilaya ya Rwamagana wamesema ya kuwa walikuwa hawajui swala hilo ila wanakwenda kufuatilia na wakikuta ni kweli watawasiliana na kituo cha RDB wenye kuwa na majukumu hayo ili wanyama hao wasiongeze kuharibu mimea ya wakaaji.

Haiko katika tarafa ya Gishari panapo semekana viboka pekee na katika wilaya ya Gatsibo, tarafa ya Kiramuruzi nao wanavamiwa na viboko kutoka katika ziwa Muhazi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leki/bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.