kwamamaza 7

Gisagara:Wakazi wapata hasara kufuatia mmomonyoko wa ardhi kutoka kambi ya wakimbizi

0

Wakazi wa tarafa ya Mugombwa wenye mashamba karibu na kambi ya wakimbizi asili ya DR Congo wameweka wazi kupata hasara kufuatia mmomonyoko wa ardhi unaosababishwa na maji kutoka kambi hii ya Gihembe.

Wakazi wametangazia VOA kuwa maji kutoka kambi hii yaliharibu mazao yao kama vile mahindi mihogo,maharagwe na migomba  na hata mashamba yao na kuwa hawana imaani kulima mashamba yao tena kulingana na alivyoharibika.

Mmoja wao amesema” Tulikuwa na mashamba yenye mahindi, mihogo,mboga na migomba lakini maji kutoka kambi yalikuja na kuharibu haya yote”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wakazi wamependekeza kuhamishwa ama kulipwa fidia ya mazao ya mashamba yao na kuwa kinyume na hili wanatarajia kuishi katika hali ya njaa. 

Diwani wa Gisagara,Jerome Rutaburingoga amesema kuwa kunafanywa takwimu za yaliyoharibika na kuwa pamoja na wadhamini wakiwemo wizara ya wakimbizi nchini na HCR ,suala hili litatolewa suluhisho hivi karibuni.

Suala hili lilitiwa hadharan na wakazi wa eneo hili mwezi Juni 2017 ila halikutatuliwa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.