Swahili
HABARI

Gisagara : Wanawake ni mfano wa maendeleo

Wakaaji na viongozi wa wilaya ya Gisagara wasema kuwa maendeleo yao huonekana kupitia wanawake, kwa mtazamo wakilinganisha namna walivyo kuwa mbele na jinsi walivyo sasa katika maendeleo ya wilaya yote.

Rutaburingoga Jereme kiongozi wa wilaya Gisagara, amesema kuwa maendeleo ya wanawake imeshangaza wengi, eti: “wanawake ni kama wanaume kwa kuelewa na kusikia, wanafanya kazi kwa umoja katika makundi”.

Yaliosukuma wanawake kuonekana katika maendeleo ya ajabu ni kuwa walifanya kazi katika makundi, viwanda na biashara kibinafsi hata kuna mwanamke ambaye ana gari ya aina ya DAIHATSU, na yeye mwenyewe huendesha gari lake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mukanyabyenda Constance ni mama wa watoto 4, ana umri wa miaka 46, anawasaidi wanawake wengine kwa kutwaa mizigo yao kwa gari lake, yupo na kiwanda cha pombe ijulikanayo kwa jina la “Inyamamare” na aliwapa watu wengi kazi.

Kiwanda chake hufanya pombe kutoka ndizi, na kwa sasa amepata ujuzi kwani pombe hio ya ndizi huigeuza pombe kali (liqueur) na hio alifunzwa na raia wa Corea. Anahamasisha kuwa mwaka huu atatengeneza vino nzuri.

Maendeleo katika wilaya hio ilitokana na mwanamke kwa kuwa mwanamke ni msingi wa familia ya Rwanda na kupanuka hata mahali pote.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com