Home HABARI MPYA Gisagara: Maendeleo yapiga hatua,kijiji chageuka mji
HABARI MPYA - November 27, 2017

Gisagara: Maendeleo yapiga hatua,kijiji chageuka mji

Wakazi wa wilaya ya Gisagara wametangaza kuwa kuna hatua ya mandeleo waliyoipiga kulingana na maisha yao miaka kumi iliyopita.

Viongozi na wakazi wa wilaya hii wamesema kuwa hali ya maisha yao ilibadilika tangu miaka kumi iliyopita.

Mmoja wao Dorolese Uwacu ambaye ni mkazi wa tarafa ya Ndora,30, ametangazia Bwiza.com kwamba maisha katika tarafa yao na wilaya yalibadilika kwa ujumla.Huyu amesisitiza hili kwa kutaja mambo mbalimbali waliyopata kama vile intaneti,simu za mikononi,hospitali na mabarabara na mengine.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwingine Simon Ndagijimana ambaye ni mkazi wa Mamba amesema kuwa maisha yao yalibadilika,kwa kuwa walikuwa wakiishi kwa maisha ya ufukara na kuwa siku hizi hulima mashamba yao kwa mbinu za kisasa,jambo liliongeza mavuno ya kilimo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Diwani wa Gisagara,Jerome Rutaburingoga amesisitiza haya kwa kusema kuwa hali ya maisha katika wilaya yanabadilika kila siku kwa kuwa kijiji kinageuka mji.

Diwani wa Gisagara,Jerome Rutaburingoga

Pamoja na haya,utafiti wa ofisi kuu ya takwimu(NISR)  wa mwaka 2014ulionyesha kuwa wilaya ya Gisagara ingali baadhi ya wilaya zenye ufukara nchini.

Wilaya ya Gisagara ilijitokeza kwenye nafasi ya 26 ya mkataba wa utendaji mwaka 2016/2017 baadhi ya wilaya 30 zinazounda nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.