kwamamaza 7

Gicumbi: Waliofanya kazi za kutengeneza matuta wanataka wapewe ng’ombe walizoahidiwa kama malipo

0

Baadi ya wakaazi wa wilaya ya Gicumbi wanadai kwamba walifanya kazi za kutengeneza matuta katika taraafa za Kaniga na Cyumba wakiahidiwa ng ombe kama malipo wangali wanasubiri, ikiwa inapita myaka 13 bila jibu.

Ingawa haiko rahisi kutambua idadi kamili ya walioshiriki katika kazi hii ya kutengeneza matuta kutokana na muda uliokwishapita . Mojawapo wa walioongea na Bwiza.com, walisema kwamba walikuwa wakija kutoka taraafa mbalimbali wakija kufanya kazi ya kutengeneza matuta haya wakitoka sehemu zaa Kaniga . Wakuwa wakiahidiwa na viongozi kwamba watapewa ng’ombe kama malipo lakini muda ulipoadia kukaletwa ng’ombe 50 wakapewa majawapo wa raia wengine wakaambiwa kungoja hadi wakachoka.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mukashema Marthe mojawapo wa waliofanyakazi katika uchimbaji matuta hayo alisema             “ tulifanya kazi kwa kipindi cha mwaka mzima wakituambia kwamba tunafanya kazi ambayo tutapewa ng’ombe kama malipo, na mimi nakaileta familia yote ili tuweze kupewa ng’mbe wengi , tulishinda kipindi cha mwaka tukifanya kazi na hata tukipigwa na njaa tukitarajia kupewa ng’ombe kama malipo, tulisikitika kuona baada ya kumaliza kazi wakileta ng’ombe wakalipa baadhi ya waliofanya kazi na kutuacha sisi na hakuna aliepata miongoni mwa wanafamilia tulivyo wanne kwa ujumla tu”

Na hata mwenzake anaeitwa Nsabimana Emmanuel, baada ya kuona baadhi ya waliofanya kazi hiyo wakilipwa, alikuwa vile vile na matumaini ya kwamba nao wangelipwa baadaye.

Aidha raia hawa wanasema kwamba japo wasingepewa malipo waliyoahidiwa wakapewa malipo ya aina yoyote wangeridhika.

Kwa upande wa madaraka ya wilaya ya Gicumbi wanachukuwa kazi hiyo raia waliyoifanyaya kama yenye manufaa ya jamii, na kuwaomba kutolalamikia malipo tena , kama alivyoarifu Mudaheranwa Juvenal, meya wa wilaya ya Gicumbi.

Akasema “ sikuhisi kwamba kungekuwa na malipo ya aina yoyote ambayo angetoka kutoka ngazi za juu kwenda kupewa wale walotengeneza matuta kwenye mashamba yao, kwa hiyo hawangelalamikia malipo , na kwa wale ambao hawajaelewa tutaendelea kuwaeleza kwamba kazi waliyoifanya walikuwa wakiifanya kwa manufaa yao binafsi kwa kuwa waliifanya mshambani mwao”

Ingawa meya asema hivi, baadhi ya raia waaliofanya kazi hiyo ya kutengeneza matuta walidai kwamba hawakuwa wakiifanya mashambani mwao kwa kuwa waliyatengeneza matuta haya katika taraafa za Cyumba na Kaniga wakitoka sehemu mbali mbali hadi mjawapo kushinda usiku hapo hapo kutokana na kwamba nyumba zao ziko mbali

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy/bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.