Home HABARI Gicumbi: Malalamiko dhidi ya huduma mbaya za hospitali ya Byumba
HABARI - SIASA - June 19, 2017

Gicumbi: Malalamiko dhidi ya huduma mbaya za hospitali ya Byumba

Baadhi ya wanaotaka huduma za hospitali ya Byumba iliyoko wilaya ya Gicumbi walalamikia huduma mbaya wanazopata wakienda kutafuta matibabu.

Watu hawa wanadai kwamba huwakuta baadhi ya wauguzi wakiwa wakiongea kwenye simu na wakalazimika kuwangojea kwa muda mlefu na kwa hii wanaomba ngazi husika kuchukulia hatua suala hili.

Katika mahojiano na Bwiza.com, mmoja wa wanaotaka huduma za hospitali ya Byumba amesema kwamba kuna wakati wanapokwenda kutafuta matibabu kwenye hospitali na wasipewe huduma kama ipasavyo badala yake wakalazimika kukaa na kungojea hadi wakakosa kuhudumiwa.

“ Nilimpeleka mke wangu aliyekuwa karibu kujifungua kwenye hospitali ya Byumba na kwa kuwa hakuhudumiwa haraka kwa uzembe wa wahudumu ilimfanya kujifungua mtoto akiwa na matatizo, mke wangu alifikia hospitali katika masaa ya moja na alingoja hadi saa kumi na moja ili aweze kuhudumiwa, na namjua mwanamke aliyefariki wakati huo” Nsanzima Eric asema

“Mimi na wenzangu huwa tunafanya safari ndefu tukija kutafuta matibabu kwenye hospitali hii, ila kunakuja wakati ambapo tunakosa wauguzi wakutuhudumia” Ingabire Nadine naye asema.

Mkurugenzi wa hospitali ya Byumba, Daktari Twizeyimana Jean de Dieu, anasema kwamba huduma mbaya wanazopewa wagonjwa wanaotaka matibabu kwenye hospitali hii zinatokana na kwamba kuna idadi ndogo ya madaktari na wauguzi kwenye hospitali wakati wanawapokea wagonjwa wengi kutoka tarafa tofauti za Gicumbi.

“kuwepo kwa suala hilo kunatokana na wingi wa wagonjwa tunaowapokea, ila tuna pia uhaba wa mahabara. Tunafikiria jinsi ya kuwakuta na kuwatibia kwenye vituo vya afya vya karibu na kwao bila kuhitajika kufikia hapa” asema.

Akihojiwa kuhusu wauguzi wanaokosa kuwahudumu wagonjwa kama ipasavyo wakiwa wakiongea kwenye simu, daktari huyu alisema kwamba atalifuatilia suala hili na ikiwa kuna yeyote atakayepatikana na kosa hili atachukuliwa hatua.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wizara ya Afya imetangaza kwamba tatizo la huduma mbaya, wanazolalamikia wagonjwa kupewa karibu nchini kote, zinatokana hususani na uhaba wa wauguzi na madaktari kwenye vituo mbali mbali vya afya na hospitali. Wizara inasema kwamba itatafuta mbinu za kuwaongeza wauguzi na madaktari katika vituo vya afya na hospitali.

Kuhusu suala la kuwaongeza madaktari na wauguzi, ni muhimu kuwaza jinsi ambayo itafanywa wakati ambapo kuna masuala kadhaa yanayodaiwa kuwepo kwenye sekta ya afya ikiwemo mtihani wanaopewa wanafunzi kabla ya kuruhusiwa kutumika katika taaluma za afya .

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.