kwamamaza 7

Gicumbi: Kinyarwanda ni hatari kwa matokeo ya mtihani kwa wanafunzi wa eneo linalotumia “Rukiga’

0

Wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Gicumbi wanaonyesha wasi wasi wa kusumbuliwa na Lugha ya Kinyarwanda kwenye Mtihani wa darasa la sita la shule za msingi.

Wanafunzi kutoka shule zilizoko karibu na mpaka wa Uganda huwa wanatumia sana Rukiga na kwa hiyi wakakichukua Kinyarwanda kuwa kigumu kuliko Rukiga.

“tunakifunza Kinyarwanda kikitusumbua kwa sababu huwa tunatumia sana Rukiga na hii kutufanya kufeli somo la Kinyarwanda katika mtihani” Benimana Emmanuel asema.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Na hata walimu wa hawa wanafunzi wakiri kwamba Kinyarwanda ni somo linalowasumbua kwa kiwango fulani. Wanasema kwamba ingawa wanafanya juhudi zote kuwasaidia, wanafunzi hao hawakosi kusumbuliwa na lugha hiyi na mwishowe kuathiri matokeo yao ya mitihani.

Mkurugenzi aneyehusika na masuala ya elimu kwenye wilaya ya Gicumbi anasema kwamba tatizo hili linajitokeza sana kwa wanafunzi wa shule za msingi wa darasa la kwanza hadi la tatu.

La hasha, ameongeza kwamba kuweko kwa Lugha ya Rukiga hakungekuwa tatizo kwa sababu kuna walimu wanao wajibu wa kuwasaidia wanafunzi hao.

Tatizo hili la watoto wanaokuta matatizo kujifunza Kinyarwanda linajitokeza sana katika maeneo ya nchi zinazopakana na Rwanda.

Aidha, Serikali ya Rwanda imejitolea lengo la kuitia nguvu lugha ya Kinyarwanda, na kwa hiyi wizara ya Elimu imeichagua kama Lugha inayopaswa kufundishwa katika shule zote za nchi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.