kwamamaza 7

Gen James Kabarebe awashirikisha vijana historia ya kujikomboa

0

Waziri wa ulinzi Jenerali James Kabarebe aliwashirikisha vijana mateso na vurugu walikutana nazo wakati wa kuikomboa nchi. Vijana hawa wanaokuwa katika masomo ya uraia katika kambi ya wanajeshi, Gabiro; wamehamasishwa kutobanwa na historia ambazo wao pekee hawakushiriki ndani.

Kabarebe amesema leo 13 Disemba 2016 wakati wa kuisha masomo haya ambayo vijana zaidi ya 700 wa ndani na wale wa nje ya nchi wameshiriki.

[ad id=”72″]

Ushahidi wake ulikuwa na lengo ya kuwakumbusha vijana wanyarwanda kwamba kuzungumza kuhusu historia ya Rwanda, ni njia nyofu ya kuimarisha umoja na maendeleo ya wanyarwanda. Alisema kwamba vita vya kujikomboa vilikuwa vigumu lakini walishinda kwa ajili ya kuweka nguvu na fikra pamoja.

Akisema kuhusu mateso walikutana nayo amesema; “Mnamo mwaka wa 1982, nilikuwa naishi karibu na kambi hii ya Gabiro kama mkimbizi katika nchi yangu ya kizazi. Serikali ya Uganda ilikuwa imeishatufukuza hivi na uongozi wa Rwanda ukisema kuwa nchi imejaa hakuna mahali pengine pa kuishi.”

abanyeshuri
Vijana katika masomo ya uraia wakisikiliza ujumbe wa waziri

Kwa upande wa vijana, wamekumbushwa kwamba janga lililotokea nchini Rwanda lilisababishwa na uongozi mbaya; na vijana walishiriki kwa kiwango cha juu katika mauaji ya kimbari. “Nchi imeharibiwa na vijana na pia ndio walihusika na majengo ya nchi.”

Viongozi wengine hasahasa mawaziri, jana walitoa  ujumbe na ushahidi kuhusu maisha yao kabla na baada ya tukio la mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mnamo mwaka wa 1994. Miongoni mwa viongozi hao kuna waziri wa vijana na mawasiliano ya teknolojia Jean Philbert Nsengimana, Gavana wa mkoa wa kusini Marie Rose Mureshyankwano; na Waziri wa utawala wa ndani na serikali za mitaa Francis Kaboneka.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.