kwamamaza 7

Gatsibo:Vijana watatua suala la mahari

0

Vijana wakazi wa tarafa ya Kiramuruzi,mashariki mwa nchi wametangaza kuwa walitatua suala la mahari.

Mmoja wao ametangazia VOA mbinu tofauti za kupata mchumba bila kulipa mahari zikiwemo kufunga ndoa bila kufanya sherehe ya harusi na kupata mkopo.

Huyu amesema kuwa kunalipwa mahari yenye kiwango cha juu,jambo lisilohusiana na hali ya msimamo wa mali siku hizi nchini.

Wazazi wa eneo hili wamesema kuwa haifai kuzuia upendo wa wanawao juu ya mahari kwa kuwa inwezekana kulipa mahari baadaye .

[xyz-ihs snippet=”google”]

Afisa wa idara ya utamaduni kwenye baraza la kutetea  lugha na utamaduni nchini,Dk. Jacques Nzabonimpa amewashauri wazazi kukumbuka maana yake mahari kulingana na mila na utamaduni.

Dk.Nzabonimpa amesema”Wazazi hawana budi kukumbuka kuwa mahari ni kama zawadi ya malezi bora,kumbukumbu,siyo vizuri mahari kuwa kipingamizi kwa bwanarusi na mchumba wake”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Haya ni baada ya vijana wengi nchini wanaotaka kupata jiko kulalamikia kiwango cha juu cha mahari wanacholipa kuwa kinaathiri maisha ya familia mpya baada ya harusi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.