kwamamaza 7

Gasabo:Mwinjilisti na mke wake washtakiwa kutesa kimwili mtoto wa miaka 4

0

Mwendesha mashtaka mkuu wa wilaya ya  Gasabo amepeleka kesi mahakamani akiwashtaki mtume wa mungu na mke wake wanaoishi kijijini Kamashashi, tarafa ya Rusororo kwa kumtesa kimwili mtoto changa wa miaka 4 aliyezaliwa nje ya ndoa na mtume wa mungu huyu.

Mwendesha mashtaka amesema kuwa  mwinjilisti  huyu alienda kumtembelea mtoto wake na kuomba mama yake kwenda naye,alipofika kwa mama wa kambo mtoto huyu aliteswa sana kwa kumtia karantini wakati wa miezi 9 bila kukanyaga nje na kukata mawasiliano yoyote na mama yake. Watuhumiwa hawa ili kuweza kuficha mabaya yao walibadili makazi na kuenda mahali pengine.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Baada ya hizi habari kuenea,mwendesha mashtaka alimkuta mtoto kwa baba yake akiwa chumbani  katika hali ya upweke ,uchafu  na majeraha mwili mzima  na sasa mtoto huyu ni mgonjwa mahtuti katika hospitali ya CHUK.Watuhumiwa wamefungwa kwenye kituo cha polisi ya Rusororo lakini wanakana kosa hili.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.