kwamamaza 7

Gasabo: Raia wanajenga stesheni ya polisi

0

Kazi ya umma ambayo ilifanyika mwezi nenda tarehe 25 Februari, raia karibu 2000 wa viini ya Gacuriro na Kagugu wilaya ya Gasabo walianza kitendo cha kujenga stesheni ya polisi.

Makamu wa kiongozi wa wilaya anayehusika na uchumi Mberabahizi Raymond alikuwepo na ndie alikua kiongozi maalum pamoja na kiongozi wa polisi katika wilaya ya Gasabo Senior Superintendent (SP) Valens Muhabwa, kiongozi wa kata ya Kinyinya na viongozi wa msingi wa kata  hio.

Jiwe la msingi ni katika kijiji ya Bukinanyana, kiini ya Nyagatovu kata ya Kinyinya na hapo ndipo kwenye kuwa kikao na wakati majenzi yatakwisha ya mbele itakuwa makao ya polisi.

Makamu kiongozi wa wilaya Mberabahizi eti:” hii ni mipango ya wilaya ya Gasabo, kila kata sherti iwe na kikao cha polisi kwa kuwa ni mafanikio kwa wakaaji wetu”.

Kiongozi wa polisi katika wilaya ya Gasabo aliwashukuru wakaaji kwa uhusiano mwema na polisi katika mambo tofauti pakiwemo kulinda usalama na kuzuia makosa.

SSP Muhabwa eti:” Polisi inashukuru nguvu munazo zitumia katika matendo pakiwemo jengo ambalo polisi hutumia katika kata tofauti za wilaya ya Gasabo, itasaidia katika mipango ya polisi na kutoa huduma nzuri tena haraka”.

SSP Muhabwa  kwa kumalizia alisema ya kuwa hao yote ni kutafuta suluhisho na uwezo pakiwa lengo la maendeleo na hio ni moja ya usamini ya Wanyarwanda na aliwaomba kuendelea na uhusiano katika maendeleo na kuulinda usalama.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.