kwamamaza 7

Gakenke: Waliodhaniwa kufa katika chimbo la madini wanusurika

0

Watu watatu waliodhaniwa kufia kwenye chimbo la migodi wanusurika baada ya kukaa shimoni kwa kipindi zaidi ya masaa 24.

Katibu mtendaji wa tarafa ya Rusasa ametangaza kwamba chanzo cha kifo hiki ni mashine ya kupakua maji iliyosababisha ajali hii ya watu kuzama kwenye chimbo hilo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kulingana na habari zilizotangazwa na Redio 1 ya Rwanda ni kwamba watu hawa wametolewa kwenye shimo hilo wakiwa wazima baada ya kushinda pale masaa 24.

Uwimana Catherine, Makamu Meya wa wilaya ya Burera anayejadili maswala ya ustawi wa jamii amethibitisha habari hii ya watu walionusurika ajali hii kupitia laini ya simu “na mimi nimepata habari hizo kijuujuu sijakuwa na habari kamili acha labda niwapigie simu watu wa hospitali inayowahudumia na nijue hali yao ya maisha”

Tatizo la uchimbaji migodi kwa njia isiyo halili limepigwa marufuku na serikali ya Rwanda huku ikiwataka watu au mashirika yanayofanya shuguli hizi kuwa na kibali cha serikali na hata vifaa vya kitaluuma.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

 

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.