Swahili
Home » Fikra zazuka mitandaoni baada ya  kiongozi mmoja kutoa hoja kuhusu bin Rais Kagame
HABARI

Fikra zazuka mitandaoni baada ya  kiongozi mmoja kutoa hoja kuhusu bin Rais Kagame

Fikra mbalimbali zimezuka kwenye mitandao ya kijamii hasa wa twitter baada ya Kiongozi wa ‘Itorero’ nchini Rwanda, Edouard  Bamporiki  kuonyesha kuwa amefurahishwa na mafanikio ya bin Rais Kagame kwa jina la Ivan Cyomoro Kagame.

Bamporiki amekosolewa alipojibu alichoandika binti Rais Kagame kwa jina la Ange Kagame kwenye twitter akimpongeza nduguye Ivan kwa kumaliza masomo ya chuo nchini Marekani.

Alichoandika binti Rais Kagame

Akiandika kwenye twitter yake,Bamporiki ameandika kuwa mafanikio ya Ivan ni jambo  lakujivunia kwake na ni muhimu kwake na  kwa jamii kwa ujumla.

“Anastahili kupongezwa!Bila shaka ujuzi aliovuna utaletea faida jamii kwa ujumla”

Mawazo ya Edouard Bamporiki na ya Manzi Twizere kwenye twitter

Kwa upande mwingine, mmoja mwa watumiaji wa Twitter kwa majina ya Twizere Manzi amemkosoa  kwa kumuambia analofanya ni kujipendekeza.

Twizere Manzi ameandika” Uku ni ugucinya inkoro kumaanisha Haya ni kujipendekeza”

Punde si punde,Edouard Bamporiki amemjibu Twizere kwa kumuuliza pilipili asiyoila yamuashi yani

“Mbona  najipendekeza na wewe ukaumia” Bamporiki akajibu

Edouard  Bamporiki alikuwa mbunge kabla ya kuteuliwa kiongozi wa ‘Itorero’  nchini.Ni  mwanzilishi wa mpango wa serikali kwa jina la ‘Ndi Umunyarwanda’ unaolenga kuleta umoja kati ya Wanyarwanda.

Mala nyingi anakosolewa na wapinzani wa serikali ya Rwanda wakimshtaki kujipendekeza na mambo mengine.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song update

 

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com