kwamamaza 7

FERWAFA yafafanua vuguvugu iliyomo na kiongozi wake De Gaulle

0

Kupitia tangazo linalohusu viombo vya habari, FERWAFA imesema kuwa bodi kuu yake wamemuandikia  Nzamwita De Gaule ikimuomba maelezo kuhusu matumizi ya  fedha kama ilivyosisitizwa na kiongozi mkuu wa CAF,Ahmed mwezi wa Machi 2017

Kiongozi wa shirika la kandanda nchini Rwanda (FERWAFA),Nzamwita Vincent de Gaulle

Kwa hiyo,FERWAFA inaeleza kuwa ilipokea $100,000 kutoka CAF yakiwemo $20,000 za kiongozi,$50,000 za kukuza mpira wa miguu wa watoto na $30,000 za kusaidia wapuliza vipenga na kuwa hizi fedha za kiongozi zilisambazwa miongoni mwa washiriki wa FERWAFA .

Pengine FERWAFA imeleza kuhusu ushuru wa fedha $20,000 De Gaulle alizozipokea kuwa katibu mkuu wa makamu wa FERWAFA alimshauri de Gaulle kuwa haiwezekani  FERWAFA kulipa ushuru wa fedha alizozipokea baali ni yeye mwenyewe atakayelipa.Taarifa hizi zinaeleza kuwa de Gaulle aliomba  ushauri wa Ofisi kuu ya ushuru nchini Rwanda (RRA) wa kuwa atalipa ushuru kisha apeleke ankara kwenye kituo cha CAF ili aziludishiwe fedha alizozitumia.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa hii inaongeza kwa kusema kwamba Vincent  De Gaulle hakuamua peke hata jambo moja kwa kuwa maamuzi yote wakati wa miaka 4 akiwa madarakani yalikuwa yakitolewa na kamati kuu kwa ujumla na kuongeza kuwa bodi kuu ya uongozi wa FERWAFA haina uwezo wowote wa kumuomba maelezo kuhusu lolote kwa hiyo wanayotaka kujua  wataelezewa kwenye kamati kuu ya FERWAFA.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.