Home HABARI FARDC katika malumbano na wanamgambo wa Mai-Mai
HABARI - June 17, 2017

FARDC katika malumbano na wanamgambo wa Mai-Mai

Asubuhi ya Ijuma ya tarehe 17/6 kumetokea malumbano kwenye eneo la Kalunguka na Pambuka katika Teritwari ya Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya FARDC(jeshi la Congo) na wanamgambo wa Mai-Mai.

Malumbano hayo kama ilivytangazwa na Msemaji wa Opereshini ya Kijeshi ya Sokola 1, Lt Jules Ngongo, yametokea pindi ambapo wanajeshi wa FARDC walipokuwa wakiwakimbiza waasi walioshambulia maeneo ya Kabasha na Mukulia Alhamisi hii.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa upande wa Shirika la Jamii katika eneo la Beni wamesema, kwa mjibu wa Redio Okapi iliyotangaza habari hii kwamba wanachoka na mashambulio ya hapa na pale ya makundi ya waasi kwa kuwa inawafanya wakazi wengi wa maeneo karibu ya mji wa Beni kupoteza maisha.

Shirika hili linaomba pia jeshi la serikali kuwashambulia na kuwafukuza katika kambi zao.

Eneo hii la mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linakaliwa na makundi kadhaa ya waasi ambao huwa wakifanya mashambulizi ya hapa na pale na kuwaua raia na hata kupora mali yao. Siku za hivi karibuni kurilipotiwa pia malumbano kati ya kundi la mai- mai na wanyamulenge.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.