kwamamaza 7

Familia ya mfalme Kigeli V Ndahindurwa wametangaza siku ya mazishi

0

Familia ya mfalme Kigeli V Ndahindurwa, aliye fariki tarehe 16 Oktoba 2016, wametangaza yanayo husiana na mazishi ya mwili wake.

Kwenye maongezi na watangazaji habari jana tarehe 11 Januari 2017, Mchungaji Ezra Mpyisi aliye sema kwa jina la familia kwamba mazishi yatafanyika Juma pili tarehe 15 Januari mwaka huu. Alisema kua mwili wa mfalme utazikwa Nyanza sehemu ijulukanyo kwa jina la Mwima karibu ya kaburi ya Mutara III Rudahigwa.

[ad id=”72″]

Familia hio imepinga vikali kitendo kilicho itwa kua kuna yule aliye teuliwa tena kama mfalme aliye tangazwa na msemaji wa Kigeli V, Boniface Benzige.

Pasta Mpyisi pamoja na familia ya mfalme walifanya uchunguzi na hakuna yule mfalme alitangaza kua atakuwa mwakilishi wake, kwa hayo wataketi pamoja kama falimilia wajongelee serikali na kuona la kufanya na ndipo watatangaza.

Kigeli V Ndahindurwa alizaliwa tarehe 29 Juni 1936, akatawala tangu tarehe 25 Julai 1959 hadi Januari 1961, wakati alipo kimbizwa katika nchi ya Tanzania nyuma ya hapo akakwenda Marekani 1992, na alifariki tarehe 16 Oktoba 2016 na mwili wake ukafikishwa Rwanda tarehe 9 Januari 2017.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.