kwamamaza 7

Familia kupelekwa mahakamani kwa ukosefu wa majukumu

0

 

Katika wilaya ya Gicumbi, mkoani kaskazini wametoa uamuzi juu ya familia zenye kuwa na watoto wenye uchafu na kuzurura barabarani zinatakiwa kuperekwa mahakamani ili kuwaamsha wazazi juu ya ukosefu wa majukumu. Mwito ulitolewa juzi katika sherehe za sikukuu ya mwanamke wa kijijini.

Uongozi wa wilaya umechukuwa hatua ya kupambana na tatizo la migogoro inayojitokeza katika familia na kusababisha watoto kuondoka nyumbani na kuzururazura barabarani. Uamuzi huu utakuwa sambamba na kupambana na tatizo la uchafu.

Meya wa wilaya ya Gicumbi, Mudaheranwa Juvenal alisema kwamba wazazi wanaokosa majukumu wanatakiwa kuperekwa mahakamani.

“Hakuna sababu ya kutolea watoto wenu vizuri,…mtaitwa mahakamani, ni lazima kujua kwamba hakuna mtoto aliyezaliwa ili aishi barabarani. Ilikuwa onyo, msishangae tukiziita familia hizo kwenye kituo cha polisi”. Meya Mudaheranwa Juvenal alionya.

Wanawake wa Gicumbi walihamasishwa kufanya juu chini ili kufikilia kimaendeleo na kujiunga na shirika za fedha pamoja na kufaidikisha miradi za serikali za kuwasaidia.

Théogène U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.