kwamamaza 7

DRC: Marais waunga mkono mkataba wa kumwongeza muda rais Kabila

0

Marais wa nchi za kanda ya maziwa ICGLR na wale wa jumuiya ya SADC wameunga mkono mkataba wa kisiasa wa Kinshasa uliotiwa saini mjini Kinshasa wiki iliyopita na ambao unaongeza muda wa rais Kabila kuendelea kubaki madarakani hadi  mwezi Aprili 2018.

Marais hao wamezungumzia pia hali ya kisiasa nchini Burundi, Jamhuri ya Afrika ya kati na Sudan Kusini. Viongozi hao pia wamelaani machafuko yaliotokea jijini Kinshasa 19 na 20 Septemba mwaka huu na kutaka kuwe na amani ya kudhumu nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Agustine Mahiga katika mahojiano na VOA amesema nchi za maziwa makuu ambazo zina matatizo yanayofanana lakini Congo ni zaidi na walikuwa wakijadili nchi hiyo kwa undani zaidi.

[ad id=”72″]

Marais hao hawakueleza tofauti ya upinzani na kabila itakavyopewa ufumbuzi wakisema yale ya muhimu yanayotakiwa kwasababu ya muhimu yanaweza kuzungumzwa na kazi bado inaendelea.

Kila mtu anahusika katika hili SADC tupo karibu zaidi na DRC kwasababu ni wanachama lakini au tuko mbele zaidi baada ya kumteuwa Edem kojo kuwa msimamizo aliongeza waziri Mahiga.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.