kwamamaza 7

Dr Joseph Nkusi amefikishwa Rwanda kutoka Norway

0

Dr. Joseph Nkusi, raia wa Rwanda amefikishwa Rwanda akitoka Norway, alipenda sana kuandika sana kwenye blog yake, anashutumiwa kutosamini na itikadi ya mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi yaliyofanyika mwaka wa 1994, juma tatu ya wiki ijao atafikishwa mahakamani mjini Kagali na kuanza kujieleza kwa yale anayo shutumiwa kuhusu itikadi mauaji ya Kimbari na ubaguzi.

Mahakama ya Nkusi itakuwa muda muzuri wa kutofautisha kati ya itikadi ya mauaji ya Kimbari kama kosa la kisheria ya Rwanda na kusema unayo yafikiri ao uhuru wa kukosoa serikali ama chama tawala.

Nkusi aliishi Norway tangu mwaka wa 2009 hadi 2016. Viongozi wa Norway walikataa kumupa vitambulisho vya ukimbizi wakisema ya kuwa hawaoni sababu ya kuomba hawaoni mateso anayo weza pata akifika Rwanda na alilazimishwa kurudishwa Rwanda na ndipo akatarudishwa tarehe 8 Oktoba 2016.

Uongozi wa Rwanda walimutia mbaroni alipo fika Rwanda, akapokea maswala kuhusu maandiko yake na mambo ya siasa, hivi yupo katika gereza ya Kimironko tangu siku hio kama vile husema Rwandawire.

Mamoja Nkusi alio andika kwenye blog yake “Shikama” aliandika: kusema mauaji yalio fanyika ni mauaji ya Kimbari hakuna usamini, akisema mfano ya kuwa Watusi na Wahutu wote walikuwa wakiwindwa na alisema ni mauaji ya kimbari mara mbili (double genocide) na hayo ni tofauti na utafiti ulio fanywa na Human Rights Watch na jamii zingine.

Sheria ya Rwanda inafasiriya ya kuwa itikadi ya mauaji ya Kimbari kuwa ni tendo linalo fanyika kwenye watu wengi katika maksudi na kuonyesha ya kuwa anaishi ubaguzi wa kabila, dini, nchi ao rangi ya ngozi.

Hata kama maandiko ya Nkusi yalionekana vibaya, viongozi wa Rwanda wana uwajibu ili apate ukweli na sheria kamili na asihukumiwe kwa sababu alikosoa serikali ao chama tawala kama vile taarifa husema.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.