kwamamaza 7

Dr Habineza Frank na Mwenedata kuasilisha ugombea wao kwenye NEC

0

Mwenedata Gilbert, alietangaza nia yake ya kugombea urais wa Rwanda atawasilisha ugombea wake pamoja na Saini za watu waliompigia ,kwenye Tume ya Uchaguzi ya Nchi,Dr. Frank pia alietangazwa na Chama chake cha Green Party kwamba atakuwa mgombea nae atawasilisha ugombea wake hii leo.

Shughuli hii imeaanza leo hii saa nne tarehe 12 Juni 2017 kwenye kao kuu la Tume ya Uchaguzi lilko Kimihurura.

Bwiza.com katika mahojiano na waliwotangaza kuwa watawania kiti cha urais, moja wapo wameitangazia kwamba wamekwisha jaza idadi ya saini zinazohitajika wengine wakatwambia kuwa baado wanasubiri.

Mwenedata amesema kuwa alipata pingamizi kadhaa ambazo atazungumzia kwa kina adhuhuri ya leo, lakini bila shaka atawasilisha ugombea wake hii leo.

Akizungumzia kuhusu Uchaguzi Mwenedata amesema yuko anajiaanda vizuri na ana imani atashinda na asiposhinda ataridhika na mchango ambao atakuwa ameacha wakidemokrasi.

Kuhusu pingamizi alizozikuta hakukata tama bali alijaribu kusimama sawa sawa hadi apate saini alizokuwa anasaka.

Mpayimana Philippe yeye hajajaza saini anazohitajiwa kupata kwa kuwa hadi sasa, anabaki na wilaya tatu ambazo hajafikia kwa sababu nyingi ambazo anafafanua.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Asema “tungali na siku kumi za kupigisha saini, tarehe ya mwisho ni 23 Juni, inaeleweka tumezikuta pingamizi kadha. Mjawapo wa waakilishi wangu walikata tama na nikalazimika kuwatafuta wengine , kuna wengine waliokubali kusaini baadaye wakabadili mawazo, haikuwa njia rahisi”.

Alihusisha pingamizi hizo na wilaya tatu ambazo hajazifikia

Anasema kwamba kinachobaki ni saini hizo tu wakati atakapozipata atawasilisha ugmbea wake katika NEC.

Kwa upande mwingine, chama cha Democratic Green Party of Rwanda kimekwisha tangaza kwamba kitasimamiwa na Dr Frank Habineza kama mgombea katika Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri.

Dr Frank Habineza nae atawasilisha ugombea wake NEC hii leo.

Tumejaribu kumtafuta Shima Rwigara Diane lakini hatukumpata kwenye simu.

Watu hawa ndio waliotangaza nia yao ya kugombea kama wagombea binafsi ambao ni Shima Rwigara Diane, Mpayimana Philippe, na Mwenedata Gilbert.

Kwa upande wa vyama kuna vyama tatu vilivyomtangaza rais Kagame kama mgombea wa upande wao. Isipokuwa PL na PSD kuna chama kingine kilichoitangazia bwiza.com kwa faragha kama kitamuunga mkono rais Kagame.

wakati huu, wanaounda kamati la uchaguzi katika Chama cha RPF kwa ngazi ya Jimbo zote zikiwa nne na mji wa Kigali, walikwisha mtangaza Kagame kama mgombea wa Chama cha RPF kwa matokeo ya 100%.

NEC itaanza kupokea rasmi hii leo ugombea wa watakaowania kiti cha Urais mwezi Agosti 2017

Katibu Mtendaji wa NEC,Charles Munyaneza , amesema kwamba mgombea mwenye kukidhi vigezo ndie anaeruhusiwa kugombea .

Ugombea unaasilishwa na mtu binafsi anaetaka kuwania urais na akapewa cheti cha kuthibitisha kwamba ugombea umepokewa . Tume ya uchaguzi mpaka hapo ikakaguwa kwamba vigezo vinakidhi kabla ya kumruhusu kugombea.

Tarehe 23 Juni ndio tarehe ya mwisho ya kuwasilisha ugombea .NEC itatangaza wagombea kwa muda tarehe 27 Juni. watamtangaza pia mgombea ambaye atakuwa anakosa cheti Fulani na wampe muda wa kikitafuta hadi tarehe 7 ambayo wagombea rasmi watatangazwa. Itakuwa ikiwa mwezi mmoja tu kabla ya Uchaguzi ambao utafanyika tarehe 3 na 4 Agosti.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.