kwamamaza 7

DR Congo:Tume ya uchaguzi kutangaza kalenda ya uchaguzi leo

0

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC,CENI inatarajiwa kutoa kalenda ya uchaguzi mwishoni mwa juma hili licha ya Tume hiyo hapo awali kutoa angalizo kuwa uchaguzi hauwezi kufanyika kabla ya mwaka 2019.

Hayo yanajiri wakati huu hali ya joto la kisiasa ikiendelea kupanda kwa Rais Joseph Kabila kutakiwa kuondoka madarakani kwa kuheshimu makubaliano ya Disemba 31 mwaka jana huku Marekani ikishinikiza uchaguzi ufanyike mwaka 2018.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hivi karibuni Naibu Mwenyekiti wa CENI, Norbert Basengezi ameripotiwa akisema kuwa kalenda ya Uchaguzi itatolewa mwishoni mwa juma hili na kwamba makubaliano ya Desemba 31 yataheshimiwa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Norbert Basengezi amesema kuwa tayari tume yake imekutana na wajumbe wa kamati inayoratibu utekelezwaji wa makubaliano hayo pamoja na wajumbe wa serikali ili kuafikiana kuhusu kalenda ya uchaguzi.

Asili:RFI

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.