kwamamaza 7

DR Congo: Wanyarwanda na Warundi waliofungwa wangali hatarini

0

Wanyarwanda na Warundi waliokamatwa  eneo la Uvira, Kivu kusini kwa mashtaka ya kuwa wanamgambo wameomba msaada kutokana na hali mbaya gerezani.

Mwengi mwa hawa ni vijana ambao walikamatwa kwa mashtaka ya kuwa miongoni mwa wanamgambo dhidi ya serikali ya Burundi ikiwemo  RED Tabara na FNL.

Kwa mujibu wa taarifa za  SOS Media, Wanyarwanda pia wanashtakiwa haya mashtaka.

Hawa wafungwa wametengaza maisha yao yangali hatarini kutokana na ukosefu wa chakula kwa kudai wanakula mala moja katika siku mbili.

Hawa wanahofia kukumbwa na maradhi ya kuambukizwa, utapia mlo na  uchache wa hewa kutokana na watu wengi gerezani.

Hawa wametangaza wanahitaji msaada wa kisheria na wa maisha ya kawaida.

 

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.